Kiungo wa klabu ya Yanga sc na timu ya taifa ya Tanzania Feisal Salum “Fei toto” ameshindwa kusafiri na timu ya taifa kwenda nchini Rwanda kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya nchi hiyo(The Amavubi) baada ya kukosa hati ya kusafiria(pasipoti).
Kiungo huyo ameungana na beki Kelvin Yondani ambaye naye ameshindwa kusafiri na timu hiyo baada ya kupata majeraha na hivyo kuwafanya wote kukosa mechi hiyo pamoja na ile ya kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) dhidi ya Sudan.
Ettiene Ndayiragije ambaye ni kaimu kocha mkuu wa timu ya taifa amethibitisha kukosekana wachezaji hao huku Fei toto akisema pia licha ya tatizo la hati pia anauguliwa na baba yake mzazi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.