Site icon Sports Leo

Sarri Aondoka Chelsea

Klabu ya Chelsea imefikia makubaliano na klabu ya Juventus juu ya kocha Maurizio Sarri kujiunga na mabingwa hao wa nchini Italia “Serie A”, makubaliano hayo yamefikiwa usiku alhamisi baada ya maongezi ya vilabu hivyo viwili na dili linatarajiwa kukamilishwa mapema leo ijumaa.

Inaelezwa makubaliano hayo yamehusisha kiasi cha malipo ya £5m, itakumbukwa kocha Maurizio Sarri aliwasili katika klabu ya Chelsea July mwaka 2018 akitokea katika klabu ya Napoli na ameiwezesha Chelsea kumaliza katika nafasi ya tatu ligi kuu nchini Uingereza “Premier League” na wakishinda kombe la Europa katika msimu wake wa kwanza lakini pamoja na kusaini mkataba wa miaka mitatu July mwaka jana,Sarri atakuwa kocha wa tisa kuondoka katika klabu ya Chelsea chini ya mmiliki Roman Abramovic.

Maurizio Sarri anaondoka katika klabu ya Chelsea ikiwa umepita muda mchache tangu kuondoka kwa mshambuliaji Eden Hazard aliyejiunga na klabu ya Real Madrid na huku klabu hiyo ikiwa katika kifungo cha kutokusajili mchezaji kwa muda wa miaka miwili ya madirisha ya usajili jambo ambalo wamekatia rufaa katika rufaa katika mahakama ya michezo ya usuluhishi na wanasubilia maamuzi tena.

Kwasasa klabu ya Juventus haikuwa na kocha kufuatia kuondoka kwa kocha Massimiliano Allegri mwishoni mwa msimu uliopita, akiwa ameshinda makombe ya ligi katika kila msimu ndani ya misimu mitano aliyohudumu katika klabu hiyo tangu mwaka 2014.

Exit mobile version