Home Soka SIMBA KUIBOMOA KAGERA SUGAR, WAWILI WATAJWA

SIMBA KUIBOMOA KAGERA SUGAR, WAWILI WATAJWA

by Sports Leo
0 comments


NYOTA wawili wa Kagera Sugar, Ramadhan Kapera na Kassim Khamis wameonyesha dalili za kuihama timu hiyo itakayocheza Play off na Pamba huku Simba na Yanga zikitajwa kuonyesha nia ya kuwasajili washambuliaji
hao.
Kapera na Khamisi walikuwa msaada mkubwa katika klabu ya Kagera Sugar na kuwa mwiba mkali katika michezo mingi ya ligi kuu hasa ule wa Simba uliopigwa katika Uwanja wa Kaitaba ambapo wote walifunga bao moja moja na kuipa Kagera ushindi wa mabao 2-1.
Rafiki wa karibu na wachezaji hao, alisema wachezaji hao wanawindwa na timu nyingi zikiwemo Simba na Yanga na hali ilivyo wataachana na klabu hiyo katika wiki za karibuni.
“Unajua wale walianza kuwindwa kabla hata ligi haijafi ka mwishoni, timu nyingi sana zilionyesha nia ya kutaka kuwasajili hata hawa Simba na Yanga wameonekana kuwahitaji sana nafi kiri muda siyo mrefu wataondoka katika klabu hiyo,” alisema mtoa habari huyo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited