22
Kikosi cha Simba kimekwea pipa mchana wa leo kwenda jijini Mwanza kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Polisi Tanzania mchezo ambao utachezwa jumamosi ya June 19 kwenye dimba la CCM kirumba.
Baada ya mchezo huo kikosi hicho kitarejea jijini Dar kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara (Vpl) dhidi ya Mbeya City mchezo ambao utachezwa jumanne ya June 22 kwenye dimba la Benjamin Mkapa.
Huku wakimaliza mchezo huo wataunganisha safari ya kwenda Songea kwa ajili ya mchezo wa nusu fainali ya kombe la shirikisho (ASFC) dhidi ya Azam mchezo ambao utachezwa June 26 kwenye dimba la Majimaji.
Cc:Mitandao ya Kijamii