Klabu ya Simba sc imeingia makubaliano na Wizara ya Maliasili na Utalii, ya kuvaa jezi zenye nembo ya neno VISIT TANZANIA kwenye michezo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba ipo kundi A na timu za Al Ahly, AS Vita na Al-Merrikh na itaanza dhidi ya AS Vita siku ya ijumaa Februari 12 ugenini nchini Congo.
Simba sc inalazimika kubadili nembo ya mdhamini kutokana na kanuni za shirikisho la mpira barani Afrika kutoruhusu klabu kuwa na wadhamini wanaofanana na wale wa shirikisho hilo ambapo kampuni ya michezo ya kubashiri ya Xbet ndio wadhamini wa michuano hiyo hivyo wadhamini wa Simba sc kampuni ya Sportspesa hawapaswi kuonekana kwa sababu wanafanya shughuli moja na Xbet.