Klabu ya Simba sc leo imepaa kuelekea jijini Arusha kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Coastal Union mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini humo.
Awali mchezo huo ulipangwa kufanyika katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga lakini kufuatia bodi ya Ligi nchini kuufungia uwanja huo hivyo Coastal ambao ni wenyeji walichagua uwanja huo kama uwanja wa nyumbani.
Coastal inabidi wajipange hasa kuweza kupata alama katika mchezo huo kufuatia timu ya Simba sc kuwa na matokeo magumu hasa baada ya kutoka sare na Yanga sc huku wakiwa wamepoteza mechi mbili mpaka sasa katika ligi kuu huku wakiwa nafasi ya tatu katika msimamo.