Klabu ya Simba sc imefanikiwa kuzoa alama tatu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tabora United uliofanyika katika Mei 6 katika uwanja wa Chamazi kwa mabao 2-0 huku mwamuzi akitia fora kwa kukataa bao la wazi la Tabora United.
Simba sc ikiwa chini ya kocha Juma Mgunda ilipata bao la kwanza dakika ya 19 likifungwa na Sadio Kanoute aliyeunganisha kona ya Ladack Chasambi ambapo baada ya bao hilo Tabora United waliamka na kufanikiwa kufunga bao dakika ya 76 ambalo mwamuzi alilikataa na punde tu Edwin Balua akafunga bao la pili dakika ya 77 ya mchezo.
Tabora United ambao wanapambana wasishuke daraja sasa wamefungwa mechi zote mbili jijini Dar es salaama baada ya awali pia kufunga 3-0 na Yanga sc katika robo fainali ya Crdb Cup.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Simba sc imefikisha alama 53 ikiwa na michezo 24 ya ligi kuu katika nafasi ya tatu ya msimamo huku Tabora united ikiwa katika nafasi ya 15 ikiwa na alama 23 baada ya kucheza michezo 25 ya ligi kuu ambapo ipo katika hatari ya kushuka daraja.