Klabu ya Simba sc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa alama tatu baada ya kuifunga Mashujaa Fc kwa bao 1-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma ambapo ilishuhudiwa wingi wa mashabiki wa klabu hiyo wakifurika uwanjani hapo.
Bao pekee la mchezo huo lilifungwa dakika ya 16 na Saido Ntibanzokiza kwa penati iliyotokana na Kibu Dennis kuangushwa ndani ya eneo la hatari na beki wa Mashujaa Fc na mwamuzi kuamuru pigo hilo ambapo kipa Eric Johora alishindwa kudaka tuta hilo.
Mashujaa wakiwa na kiu ya alama tatu wakijitahidi kurudi mchezoni kusawazisha bao hilo lakini umakini wa walinzi wa Simba sc Hussein Kazi na Che Fondoh Malone waliokoa hatari zisifike kwa kipa Aishi Manula.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kutokana na ushindi huo sasa Simba sc imefikisha alama 26 ikiwa katika nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi kuu nchini ambapo Yanga sc na Azam Fc zipo kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ya Nbc.