Home Soka Simba sc Yaponea Chupuchupu

Simba sc Yaponea Chupuchupu

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc imeponea chupuchupu kukosa alama tatu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc baada ya kulazimika kusawazisha dakika za mwishoni mwa mchezo katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Simba sc ikianza na kikosi chenye mabadiliko machache kutoka kile walichofungwa 5-1 na Yanga sc ambapo kipa Aypub Lakred alianza langoni badala ya Aisha Manula huku Andre Onana akianza badala ya Kibu Dennis ambaye ni majeruhi.

Namungo Fc ikianza na kikosi chake cha kila siku ilifanikiwa kupata bao la uongozi dakika ya 28 likifungwa na Reliants Lusajo ambapo Namungo Fc inabidi wajilaumu wenyewe kwa kushindwa kutumia nafasi kikamilifu.

banner

Kipindi cha pili Simba sc ilifanya mabadiliko ya kuwaingiza Luis Miqquison na Moses Phiri ambayo yalileta kasi eneo la mbele na kufanikiwa kuswazisha bao hilo kupitia kwa Jean Baleke aliyemalizia pasi nzuri ya Phiri dakika ya 75.

Mpaka dakika tisini zinamalizika timu hizo ziligawana alama ambapo Simba sc sasa imefikisha alama 19 ikiwa na michezo nane huku Namungo Fc imefikisha alama nane katika michezo tisa ya ligi kuu nchini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited