Klabu ya Simba sc imefanikiwa kuibuka na alama tatu katika mchezo wa ligi kuu nchini dhidi ya Tabora United baada ya kupata ushindi wa mabao 4-0 katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora.
Simba sc ilifanikiwa kupata bao la mapema dakika ya 20 kwa kichwa likifungwa na Pa Omar Jobe akiunganisha faulo ya Cletous Chama baada ya yeye mwenyewe Jobe kufanyiwa faulo na mabeki wa Tabora United.
Simba sc ilipata bao la pili likifungwa na Sadio Kanoute dakika ya 36 aliyeunganisha kwa kichwa kona iliyopigwa kutoka upande wa kulia wa uwanja huo huku uzembe wa mabeki wa Tabora United ukiwapa Simba sc bao la tatu lililofungwa na Che Malone Fondoh dakika ya 60.
Usajili mpya Fredy Michael alifanikiwa kufunga bao la nne akiwachambua mabeki wa Tabora United na kupiga shuti dhaifu lililomchanganya kipa John Noble na kuandika bao la nne kwa Simba sc ambao sasa wamefikisha alama 29 katika michezo 12 wakiwa katika nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi kuu nchini.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Simba sc sasa wataelekea jijini Mwanza ambapo watawakaribisha Azam Fc katika uwanja wa Ccm Kirumba siku ya Ijumaa ya Februari 9 mchezo ambao utatoa taswira ya muelekeo wa ubingwa wa ligi kuu nchini kwa timu hizo.