Klabu ya Simba sc imeamua kuwatema nyota wake watano wa kikosi cha kwanza kutokana na kutoridhishwa na uwezo wao ikiwa ni mapendekezo ya kocha Abdelhack Benchika juu ya masuala ya kiufundi na usajili klabuni hapo.
Katika orodha ya mastaa hao ambao baadhi watatolewa kwa mkopo huku wengine wakiachwa moja kwa moja wapo Abdalah Hamis,Nassoro Kapama,Jimmyson Mwinuka,Ahmed Feruzi na Shabani Idd Chilunda.
Wale waliosajiliwa msimu huu akiwemo Chilunda,Abdalah Hamis na Nassoro Kapama watatolewa kwa mkopo huku wengine wakitemwa moja kwa moja na tayari mastaa hao walishaondolewa katika kambi ya timu hiyo ikijiandaa na michuano ya Mapinduzi hatua ya nusu fainali dhidi ya Singida Fountain Gate Fc.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Katika orodha ya mastaa wapya klabuni hapo ambao wamesajili wapo Babacar Sarr,Ladack Chasambi,Salehe Karabaka ambapo pia klabu hiyo inadaiwa kukamilisha usajili wa Edwin Balua sajili ambazo zinampa jeuri kocha Benchika kuwatema nyota hao.