Timu ya soka ya Simba sc imeibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya mtibwa sugar katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliofanyika katika uwanja wa Jamhuru mjini Morogoro.
John Bocco aliandikia Simba bao la kwanza dakika la 45 huku Nahodha msaidizi Mohamed Hussein akifunga bao la pili dakika ya 46 na kalamu ya mabao ilimalizika dakika ya 59 kwa Hassan Dilunga kuwafunga waajiri wake wa zamani.
Simba imefikisha jumla ya alama 53 na kuendelea kukaa kileleni mwa ligi kuu Tanzania bara.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.