Kocha wa klabu ya Manchester United Olle Gunnar Solskjaer ameendeleza ubabe kwa kocha wa Chelsea Frank Lampard baada ya jana kuongoza Manchester United kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa ligi kuu Uingereza.
Mabao ya United yalifungwa na Antonio Martial 45′ akimalizia krosi ya Aaron Wan Bissaka aliyempindua mara mbili beki wa Chelsea Cezar Azpillicueta na kupiga krosi iliyomkuta mfungaji.
Harry Maguire aliihakikishia United kuondoka na pointi tatu baada ya kufunga kwa kichwa kufuatia kona iliyopigwa na Bruno Fernandez.United washukuru uwepo wa mwamuzi wa Video(VAR) baada ya magoli mawili ya Chelsea kukataliwa kufuatia picha za marudio kuonyesha hayakua halali.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
United imepanda mpaka nafasi ya saba ikiwa na pointi 38 baada ya kucheza michezo 26 pointi nne ikipunguza pengo hadi kubaki pointi 4 ili iingie nafasi nne za juu (Top Four).