Baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Nigeria katika michuano ya mataifa ya Afrika (Afcon 2024) katika hatua ya 16 bora kocha wa timu ya Taifa ya Cameroon Rigobert Song amekalia kuti kavu kuendelea kuifundisha timu hiyo.
Mashabiki wengi nchini humo wameonyesha kutoridhishwa na kiwango cha timu hiyo na hivyo kusababisha kulalamika wakimlaumu Eto’o ambaye na Rais wa Shirikisho la soka nchini humo kuwa anatumia urafiki wake na Song na kushindwa kumtimua hata kama timu hiyo imefanya vibaya.
Song anaweza kuwa na wakati mgumu zaidi kuliko makocha wote waliobaki na kuna hofu kuwa anaweza kuondolewa kwenye nafasi hiyo baada pia kushindwa kufanya vizuri kwenye Kombe la Dunia 2022.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kocha huyo ambaye alitwaa ubingwa wa Afcon mara mbili akiwa mchezaji wa Cameroon, amesema bado hajafanya uamuzi wa nini cha kufanya baada ya kutolewa Afcon.