Home Soka Soslkjaer-“Pogba Haondoki Ngo”

Soslkjaer-“Pogba Haondoki Ngo”

by Sports Leo
0 comments

Mkufunzi wa timu ya manchester united Ole Gunnar Solskjaer amethibitisha kuwa kiungo Paul Pogba atasalia klabuni hapo kwa msimu ujao wa ligi kuu ya Uingereza licha ya kuvutika na uhamisho wa kujiunga na Real Madrid na Juventus.

Kocha huyo aliyeichezea man united akitokea molde fc na kufanikiwa kucheza michezo 366 na kufunga magoli 126 amethibitisha kusalia kwa Pogba klabuni hapo wakati akiongea na waandishi wa habari akiwa na timu katika kambi ya maandalizi ya msimu mpya nchini Australia.

“Ni lazima Pogba alindwe kutokana na kipaji chake na njia pekee ya kumlinda ni kuhakikisha wote kwa pamoja timu inapata mataji”.

banner

Pia kocha huyo amethibitisha kuwa ataunda timu kumzunguka staa huyu ili aweze kuonyesha uwezo wake huku akithibitisha kuwa anahitaji kusajili wachezaji wawili ama watatu huku pia atawaondoa baadhi ya wachezaji klabuni hapo huku ikitajwa Matheo Darmian,Marcos Rojo,Erick Bailly kuwa ni miongoni mwa mastaa watakaofungiwa virago.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited