Timu ya taifa ya Tanzania(Taifa stars) imeingiza mguu mmoja katika fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani ya nchi baada ya jana kuifunga Kenya(Harambee stars) mabao 4-1 katika mikwaju ya penati.
Stars ilikwenda nchini Kenya ikiwa na deni baada ya kutoa sare katika mchezo wa awali hapa nchini na hivyo kuwalazimu kutafuta ushindi au sare ya magoli ili waweze kufuzu.
Mpaka dakika tisini za mchezo zinamalizika matokeo yalikua sare na kulazimu mchezo kuingia hatua ya matuta na timu umuhimu wa kipa Juma Kaseja ulipoonekana baada ya kupangua penati mbili na kuifanya Stars kufuzu kwa ushindi wa 4-1.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kufuatia ushindi huo stars itahitaji kushinda mechi inayofuatia dhidi ya Sudan ili kujitengenezea mazingira ya ushindi.