Timu ya soka ya taifa ya Tanzania(Taifa stars) inatarajiwa kuagwa leo mchana katika kambi ya timu iliyopo katika hoteli ya Whitesand jijini Dar es salaam.
Timu hiyo inatarajiwa kuondoka kesho kuelekea nchini Misri kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya michuano hiyo ambapo itacheza michezo kadhaa ya kirafiki kabla ya kupeperusha karata ya kwanza june 23 mwaka huu dhidi ya Senegal.
Hafla ya kuwaaga wachezaji hao itaongozwa na naibu waziri wa sanaa,tamaduni na michezo Mheshimiwa Juliana Shonza ambaye atawakabidhi bendera ya taifa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Pia Tff imedhibitisha kuwa mchezaji Shomari Kapombe hatakuwa sehemu ya msafara wa timu hiyo ili kumpa muda zaidi wa matibabu ya majeraha yake aliyopata akiwa na kambi ya timu ya taifa nchini Afrika Kusini wakati wa kujiandaa na mchezo dhidi ya Lesotho.