Home Soka Stars Watua Chan

Stars Watua Chan

by Dennis Msotwa
0 comments

Mabao ya Erasto Nyoni na Ditram Nchimbi yametosha kuifikisha timu ya taifa ya Tanzania katika fainali za michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) zitakazofanyika mwakani nchini Cameroon.

Stars ilikua na kazi ya kupindu meza baada ya mechi ya kwanza kupoteza kwa bao 1-0 katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Sudan walikua wa kwanza kupata bao dakika ya 30 kupitia kwa  Amir Kamal lakini Stars walisawazisha kupitia kwa Erasto Nyoni dakika ya 50 kwa faulo na kisha kuanza kulisakama lango mpaka dakika ya 80 Ditram Nchimbi alipowainua mashabiki wa Tanzania kwa goli la pili akimalizia kazi nzuri ya Shaban Idd Chilunda.

banner

Hii ni mara ya pili kwa Tanzania kufuzu michuano hiyo baada ya kufuzu kwa mara ya kwanza ilipokua chini ya kocha Marcio Maximo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited