Kocha wa Simba sc Patrick Aussems amesema timu hiyo lazima itaongeza mshambuliaji katika dirisha dogo la usajili baada ya kugundua upungufu katika eneo hilo.
Kocha huyo alisema hayo baada ya mechi dhidi ya mtibwa sugar ambapo timu hiyo iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 licha ya kutokua na washambuliaji wake asilia John Boko na Wilker da silva ambao ni majeruhi.
Simba imekua na wakati mgumu siku za karibuni kufuatia majeraha hayo ya washambuliaji wake hali iliyosababisha kufanya vibaya katika michezo mbalimbali ikiwemo wa kimataifa dhidi ya Ud songo ambapo timu hiyo ilimtegemea Meddie Kagere ambaye aliwekewa ulinzi mnene.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.