Home Soka Taifa Stars Kuwakosa Samatta,Sure boy

Taifa Stars Kuwakosa Samatta,Sure boy

by Sports Leo
0 comments

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania(Taifa Stars) kitaingia uwanjani kuwavaa Tunisia katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afcon mwaka 2021 utakaofanyika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Stars itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa 1-0 katika mchezo uliopita nchini Tunisia hivyo ushindi pekee ndio utafufua matumaini ya Stars kwenda katika michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Kocha Ettiene Ndayiragije amethibitisha kuwakosa Nahodha Mbwana Samatta aliye majeruhi pamoja na kuingo wa klabu ya Azam Fc Abubakari Salumu naye akiukosa mchezo huo kutokana na majeraha huku mshambuliaji Adam Adam wa Jkt Tanzania akirejea baada ya kushindwa kusafiri kutokana na kukosa hati ya kusafiria.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited