Home Soka TFF Wamgomea Dante

TFF Wamgomea Dante

by Sports Leo
0 comments

Shirikisho la soka la Tanzania(Tff) limeamua mchezaji Vicent Andrew Dante kurudi katika klabu yake mara moja baada ya mchezaji huyo kugoma kujiunga na timu hiyo.

Tff imeamua hivyo baada ya kusikiliza pande zote mbili ambapo mchezaji huyo alifungua kesi ya kudai fedha zinazokadiriwa kufikia kiasi cha shilingi milioni 45 huku pia akigomea kujiunga na timu hiyo.

Yanga nao walikata rufaa wakimtaka mchezaji huyo kudai madai yake huku akifata taratibu ikiwemo kurejea mazoezini lakini baada ya shirikisho kusikiliza pande zote ndio liliamua mchezaji huyo kurejea klabuni hapo ili pande hizo mbili ziweze kumalizana kwa amani.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited