Home Soka Tff Yapewa Kiwanja Kigamboni

Tff Yapewa Kiwanja Kigamboni

by Sports Leo
0 comments

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paulo Makonda ameendelea kugawa neema kwa soka la Tanzania baada ya kuamua kuwapa eneo la ekari 15 shirikisho la soka la Tanzania(TFF) kwa ajili ya kujenga kituo cha kuendeleza soka.

Makonda amefikia uamuzi huo leo alipokua katika hoteli ya Serena wakati wa hafla ya kuichangia timu ya taifa (Taifa stars) inayoshiriki michuano ya mataifa ya Afrika(Afcon) kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39 ikiwa kama mchango wa kamati ya hamasa ya taifa stars.

Akizungumza mbele ya makamu wa Raisi Mama Samia Suluhu Hassan makonda alisema “..binafsi mchango wangu ni kuipatia Tff kiwanja cha ekari 15 ili waweze kujenga kituo cha soka na bahati nzuri Rais wa shirikisho ameniambia fedha za kujenga kituo hicho zipo kutoka Fifa”.

banner

Makonda hivi karibuni aliwapa klabu ya Yanga eneo kwa ajili ya kujenga uwanja wao wakati akizungumza katika tamasha la kuichangia klabu hiyo la “Kubwa kuliko”.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited