Home Soka Tisa Kutemwa Msimbazi

Tisa Kutemwa Msimbazi

by Dennis Msotwa
0 comments

Klabu ya Simba ipo mbioni kuachana na mastaa wasiopungua tisa katika kikosi cha sasa wakati wa dirisha dogo mwezi ujao.

Wachezaji hao watakaotemwa wengi wao itakua kwa kushindwa kuonyesha kiwango stahiki pamoja na kukosa nidhamu katika timu hiyo jambo ambalo uongozi umelikemea mara kwa mara.

Habari za ndani ya uongozi zinadai moja ya wachezaji waliokalia kuti kavu wamo Mbrazil Wilker Da Silva ambaye amekosa namba mbele nahodha John Boko na Meddie Kagere.

banner
“Ndani ya Simba kuna wachezaji kama tisa hivi wanatakiwa kuachwa miongoni mwao ni huyu Wilker kwani hajaonyesha makali yake na wapo wengine ambao wanaweza kutolewa kwa mkopo”.

Habari za kuachwa kwa baadhi ya wachezaji zimeongelewa pia na mtendaji mkuu wa klabu hiyo Senzo Mazingisa ambaye alisema suala la kuachana na baadhi ya wachezaji na la muhimu na lazima.

“Kuwaacha wachezaji ni suala linalotokea kwenye timu zote hivyo kwa sasa kunahitaji utulivu na umakini mkubwa ili kuwapata walio sahihi,” amesema Mazingisa.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited