Home Soka TPLB Yaunguruma Vpl

TPLB Yaunguruma Vpl

by Sports Leo
0 comments

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya saa 72) imezuia baadhi ya viwanja kutumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kutokana na kuwa na upungufu katika maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la kuchezea (pitch) na uzio wa ndani unaotenganisha wachezaji na washabiki (fence).

Viwanja hivyo ni Kinesi Bull (Dar es Salaam), Bandari (Dar es Salaam), Jamhuri (Morogoro), Namfua (Singida), na Mkwakwani (Tanga).

Klabu ambazo timu zao zinatumia viwanja hivyo zimepewa nafasi ya kufanya marekebisho kipindi hiki ambacho Ligi zimepisha mechi za kirafiki za FIFA au kuchagua viwanja mbadala vyenye sifa.

Vilevile klabu zimekumbushwa kuwa kwa mujibu wa kanuni, zinapaswa kupeleka viwanjani gari ya wagonjwa badala ya gari yenye kitanda kwani kanuni ya 14(2) imetaja ambulance na si gari lolote.

“Wasimamizi wa mechi vituoni wanatakiwa kuhakikisha ambulance zinapokuwepo viwanjani kama ilivyoelekezwa kikanuni. Kama huduma ya ambulance haitokuwepo wanatakiwa kuzuia mechi kuchezwa”, imeeleza taarifa iliyotolewa na kamati hiyo kwa vyombo vya habari.

Nb.Habari kwa msaada wa mtandao wa kijamii(facebook) wa Azam Tv.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited