Home Soka Uganda Wapata Kocha Mpya

Uganda Wapata Kocha Mpya

by Sports Leo
0 comments

Shirikisho la soka nchini Uganda (Fufa)  limemteua  Johnny  Mckinstry  raia wa Ireland kuwa kocha wa Timu ya taifa ya Uganda (The cranes) kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Kocha huyo mwenye miaka 34 amechukua nafasi ya Mfaransa Sebastian Desabre aliyejiuzuru baada ya timu hiyo kutofanya vyema katika michuano ya Afcon 2019 iliyofanyika nchini Misri

Kocha huyo aliwahi kuzifundisha timu za taifa za Rwanda na Sierra leone alikua akiifundisha klabu ya Saif sporting ya nchini Bangladesh.

banner

“Bila shaka kazi hii ni (kuifundisha uganda) moja ya kazi bora za kimataifa hapa Afrika kwa maana ya mwelekeo na levo ya ushindani”Alisema kocha huyo.

Kocha huyo atasaidiwa na  Abdullah Mubiru mpaka pale atakapotaja benchi lake la ufundi na atakua na kibarua cha kuhakikisha timu hiyo inafuzu fainali za mataifa ya Afrika mwaka 2021 nchini Cameroon ambapo timu hiyo ipo kundi B pamoja na Burkina faso,Malawi na mmoja kati ya South Sudan na Sychelles.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited