Mchezaji wa zamani wa Tp Mazembe na mshindi mara moja wa kombe la klabu bingwa barani Afrika Thomas Ulimwengu amekanusha taarifa za yeye kujiunga na mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu nchini Yanga sc.
Mchezaji huyo mwenye nguvu na kasi amekanusha taarifa hizo kupitia mtandao wa kijamii ambapo aliandika “Nimesikia tetesi za nikihusishwa kujiunga na timu moja ya Tanzania,Hizo taarifa sio za kweli” aliandika Ulimwengu.
Ulimwengu hivi karibuni inadaiwa amechana na timu yake ya Js Soura ya nchini Algeria baada ya kukubaliana kuvunja mkataba.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.