Bosi mpya wa klabu ya Simba sc Senzo Masingizi ameahidi kufanya usajili wa kisomi klabuni hapo ili kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika ligi kuu na michuano ya kimataifa.
Bosi huyo aliyewahi kuwa mjumbe katika shirikisho la soka la Afrika kusini amesema atahakikisha anasajili wachezaji wenye viwango vikubwa ili kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri.
“Nitasimamia suala la usajili kuona Simba inapata wachezaji wa juu ambao watakuwa na uwezo wa kuichezea timu, kuhakikisha kuwa inatwaa ubingwa wa ligi kwa mara nyingine tena, Alisema Masingizi
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Bosi huyo amefanikiwa kupata nafasi hiyo ya kumrithi Crecentious Magori baada ya kuwashinda wengine saba ambao walifanyiwa usaili na timu hiyo.