Home Soka Varane aitaka Man Utd

Varane aitaka Man Utd

by Sports Leo
0 comments

Beki wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Real Madrid Rafael Varane ameweka wazi nia yake ya kutaka kujiunga na mashetani wekundu Manchester United katika dirisha hili la majira ya joto barani Ulaya.

Mchezaji huyo ameyasema hayo kwa klabu yake ya Madrid kupitia mawakala wake akiwaambia kuwa anataka kujaribu changamoto mpya katika ligi kuu ya malkia pale Uingereza hasa katika klabu ya Man Utd ambayo ndiyo chaguo lake la kwanza.Hata hivyo Varane amesema ataiheshimu Madrid hadi pale kalbu hiyo itakapofikia makubaliano na Man Utd.

Real Madrid walijaribu kubadilisha mawazo ya Varane ambaye kabakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake ili aongeze mkataba mpya hasa baada ya kutakiwa na kocha mpya wa klabu hiyo Carol Anceloti,lakini mchezaji mwenyewe na wakala wake wameiambia United kuwa wapo tayari kupokea ofa yao hadi 2026.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited