Miamba ya soka Barani Afrika imeendelea kutawala mpira wa miguu baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya kumi 10 mtoano kufuzu michuano ya kombe la dunia nchini Qatar 2022.
Mataifa hayo makubwa yaliyofuzu hatua hiyo baada ya kila moja kuongoza msimamo katika makundi kumi ni pamoja na Algera,Misri,Morocco,Tunisia,Ghana,Senegal,Ivory Coast,Ghana,Mali na DR Congo.
Licha ya baadhi ya mataifa kama Afrika Kusini,Tanzania,Benin kuongoza makundi yao hatua za mwanzo lakini hazikuweza kufua dafu katika mechi za mwisho.
Hata hivyo mataifa kama Ghana na DR Congo yameingia kwenye shutuma za kupanga matokeo baada ya kupata penati za utata katika mechi za mwisho za makundi yao zilizowawezesha kumaliza vinara.Madai hayo yamekuwa na nguvu kutokana na timu hizo kucheza michezo hiyo katika viwanja vya nyumbani.
Kama Benin na Afrika Kusini watakata rufaa FIFA inaweza kupanga kurudiwa kwa michezo hiyo kama ilivyokuwa 2018 kwa Senegal ilipodai kufanyiwa hujuma na Afrika Kusini kwa kufungwa 2-1 na FIFA kuamuru mchezo urudiwe ambapo Senegal walishinda 2-0.