Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania limefanya mabadiliko ya viingilio katika mchezo wa Kariakoo Derby (Yanga sc vs Simba sc) ambapo katika viingilio vipya vinasomeka kama ifuatavyo.
Jukwaa la VVIP litakuwa na mualiko maalumu, kwahiyo kwa atakayehitaji kukaa Jukwaa hilo awasiliane na TFF\
Viingilio vingine ni:
VIP A – Tsh 30,000/-
VIP B na C – Tsh 20,000 badala ya Tsh 15,000 iliyotangazwa hapo awali
Viti vya Orange itakuwa shilingi 10,000/- na Mzunguko itakuwa ni shilingi 7,000/-
Mchezo huo utapigwa tarehe 8 Machi (Jumapili) katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, muda ni saa 11 jioni ambapo Yanga watakua wenyeji.