Dirisha dogo la usajili lilinataraji kufunguliwa siku ya ijumaa ya jana (Nov 15) na kufungwa December 15 mwezi ujao siku kumi kabla ya kula sikukuu ya krimasi.
Tayari Yanga SC imeanza mikakati mapema kuhakikisha inatumia dirisha hilo dogo kujenga kikosi imara kilichosheheni nyota wenye vipaji katika kila idara.
Baadhi ya nyota kama Issa Bigirimana,Mustapha Selemani,Mybin Kalengo wakiwa katika hatari ya kutemwa tayari timu hiyo yenye makao makuu mitaa ya twiga na jangwani imeanza kuwanyemelea baadhi ya mastaa kama Bakari Mwamnyeto na Ayoub Lyanga kutoka Coastal Union huku pia ikimnyatia Ditram nchimbi kuongeza makali ya safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.