Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally kuelekea mchezo wa Simba wa Ligi Kuu dhidi yq Namungo FC ametaja wachezaji ambao watakosekana katika mchezo huo.
Wachezaji hao ni Sadio Kanoute, Kibu Dennis na beki wao Israel Patrick Mwenda ambao ni majeruhi ambapo Kanoute na Kibu waliumia katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga sc uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es salaam siku ya Jumapili Novemba 5.
Simba sc inaelekea katika mchezo huo ikiwa na hasira ya kupoteza kwa mabao 5-1 dhidi ya Yanga sc katika mchezo uliopita huku tayari ikiwa imeachana na kocha wake mkuu Roberto Oliveira na timu sasa ipo kwa kocha Dani Cadena ambaye amekaimu akisaidiwa na Seleman Matola.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.