Klabu ya soka ya Singida Fountain Gate Fc imefungiwa kusajili mpaka itakapomlipa aliyekuwa mchezaji wake Pascal Serge Wawa ambaye ilimtema mwanzoni mwa msimu huu bila kufuata utaratibu na kusababisha mchezaji huyo kushtaki Fifa.
Uamuzi huo umefanywa na Shirikkisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) baada ya Wawa kushinda kesi ya madai aliyoifungua dhidi ya Klabu hiyo ambapo ilitakiwa imlipe ndani ya muda wa siku 45 tangu uamuzi huo utolewa lakini klabu hiyo haikufanya hivyo.