Home Soka Wiki ya Mwananchi Sasa Septemba 12

Wiki ya Mwananchi Sasa Septemba 12

by Dennis Msotwa
0 comments

Klabu ya Yanga sc imetangaza rasmi kufanya tamasha lake la kila mwaka maarufu kama wiki ya mwananchi Septemba 12 2025 katika uwanja wa Benjamini Mkapa ambapo itaambatana na burudani mbalimbali pamoja na mechi ya kirafiki ya kimataifa.

Katika siku hiyo maalumu ya utambulisho wa mastaa wa kikosi hicho hasa waliosajiliwa msimu huu utafanyika ambapo pia watawaona mastaa hao wakicheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ambayo haijatajwa mpaka pale uongozi wa klabu hiyo utakapothibitisha rasmi.

Wiki ya Mwananchi Sasa Septemba 12-sportsleo.co.tz

banner

Tamasha hilo litafanyika siku hiyo ikiwa ni siku ya ijumaa siku mbili baada ya kufanyika kwa tamasha la Simba day ambalo hufanywa na watani zao Simba sc huku matamasha yote yakiwa na dhima zinazofanana.

punde tu baada ya tamasha hilo siku nne mbele septemba 16 timu hizo zitavaana katika mchezo wa kufungua pazia la ligi kuu ya Nbc nchini ambapo zitacheza mchezo wa ngao ya jamii wenye lengo la kurudisha kwa jamii kwa kupeleka misaada mbalimbali ambapo mchezo huo hua na kombe uwanjani.

Tamasha hilo litajumuisha wasanii watakaotoa burudani mbalimbali huku ikiwa na juma zima la kufanya shughuli za kijamii ikiwemo kutoa misaada,kufanya usafi wa mazingira na kuchangia damu ikijumuisha mashabiki na wanachama wa klabu hiyo ambao huwa na utaratibu wa kujitokeza kwa wingi zaidi.

Misimu kadhaa iliyopita Yanga sc imekua na muendelezo mzuri wa tamasha hilo ambapo idadi kubwa ya mashabiki imekua ikijitokeza sambamba na burudani mbalimbali zikikonga nyoyo za mashabiki akiwemo staa Koffi Olomide aliyewahi kuwa mtumbuizaji mkuu katika hafala hiyo miaka miwili iliyopita.

Pia ujio wa timu kama Kaizer Chiefs katika tamasha hilo miaka miwili iliyopita ilileta chachu ya mashabiki kuwa na shauku ya kuhudhuria kwa wingi ambapo msimu uliopita ambapo timu ya Red arrows kutoka Zambia ilikua mgeni mwalikwa ambapo ilikubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa wananchi.

msimu huu mashabiki wa Yanga sc wana hamu ya kuwaona mastaa kama Offen Chikola,Mohamed Doumbia,Celestine Ecua,Moussa Bala Conte,Andy Boyeli,Abubakar Nizar Ninju,Abdulnasir Othman Casemiro,Lassine Kouma na Mohamed Hussein Zimbwe aliyesajiliwa kutoka Simba Sc.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited