Mkurugenzi wa uwekezaji wa GSM Hersi Saidi amebainisha kwamba hivi karibuni klabu ya Yanga itasaini Mkataba wa ushirikiano na klabu moja kubwa kutoka nchini Hispania.
Kwa mujibu wa injinia huyo klabu hiyo iko kwenye viwango vya nafasi (4) za juu kwenye ligi kuu nchini humo yaani Laliga.
Pia amebainisha kuwa Mkataba huo utakuwa wa kushirikiana na klabu ya Yanga katika program za mazoezi, Vyumba vya kubadilishia nguo (dressing room), aina ya vifaa vitakavyo tumika mazoezini, ufundishaji,Kutafuta vipaji(scouting ).
Licha ya kugoma kuitaja ambapo Amesema klabu hiyo itawekwa hadharani hivi karibuni baada ya baadhi ya mambo muhimu kukamilika.