Sports Leo

Yanga Ndani ya Kagame Cup Rwanda

Timu ya Yanga Sc imepokea mwaliko kutoka shirikisho la soka la Afrika mashariki na kati (cecafa) kushiriki katika mashindano ya kombe la kagame kwa mwaka 2019 yatakayofanyika nchini Rwanda.

Katika barua hiyo ya mwaliko iliyosainiwa na katibu mkuu wa cecafa Nicholaus Musonye imeitaka yanga kudhibitisha ushiriki wake katika michuano hiyo itakayofanyika julai mwaka huu.
Ikumbukwe michuano hiyo hudhaminiwa na Raisi wa Rwanda Paul Kagame na hushirikisha washindi wawili wa juu wa kila ligi pamoja na timu waalikwa.

Exit mobile version