Home Soka Yanga Sc Kumtambulisha Guede Rasmi

Yanga Sc Kumtambulisha Guede Rasmi

by Dennis Msotwa
0 comments

Mabosi wa klabu ya Yanga sc wamepanga kumtambulisha mshambuliaji mpya wa klabu hiyo Joseph Guede katika mchezo wa kombe la shirikisho jioni ya leo Januari 30 itakapokutana na timu ya Hausing Fc ya Njombe katika mchezo wa kiporo wa kufuzu hatua ya 32 ya michuani ya Azam Sports Confederations Cup katika uwanja wa Chamazi.

Yanga sc tayari ilishawatambulisha Shekhan Ibrahim pamoja na Augustine Okrah kupitia michuano ya kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar na leo mashabiki watapata wasaa wa kumuona mshambuliaji huyo ambaye alisajiliwa siku ya mwisho ya usajili wa dirisha dogo.

Katika mchezo wa leo Yanga sc itawakosa Djigui Diarra na Stephane Aziz Ki ambao wapo katika michuano ya mataifa ya Africa inayoendelea nchini Ivory Coast ambapo timu hizo zitakutana kesho kuwania hatua ya kuingia robo fainali ya michuano hiyo.

banner

Pia timu hiyo ipo katika harakati za kutetea ubingwa wa michuano hiyo ambayo waliichukua ubingwa msimu uliopita baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya Azam Fc kwa bao 1-0 katika fainali iliyofanyika mkoani Tanga katika uwanja wa Mkwakwani.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited