Afisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema tayari mshambuliaji huyo amelipwa stahiki zake zote pamoja na gharama za mawakili wake kama ilivyoelekezwa na FIFA..
“Napenda kuwathibitishia Wananchi kwamba tumemalizana na Tambwe, klabu imefanya malipo yote yaliyotakiwa kwa mujibu wa maelekezo hivyo hatudaiani chochote na Tambwe,” amesema.
Amesema Yanga imelipa jumla ya Dola za Kimarekani 22,791 ambazo ni sawa na Shilingi 52,603,000 za Kitanzania.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
“Kati ya pesa hizo dola 21,161 za Kimarekani ambazo ni sawa na Shilingi 48,840,900 hizi ni za deni la Tambwe na Dola 1630 ambazo ni sawa na 3,762,140 gharama za mawakili, hivyo Klabu iko huru kwenye adhabu iliyokuwa imewekwa kwenye agizo la malipo hayo,” amesema Bumbuli.