Home Soka Yanga Sc Yatuma Malalamiko Caf

Yanga Sc Yatuma Malalamiko Caf

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga SC ikiwa imepita siku moja tangu itolewe katika michuano ya CAF Champions League hatua ya robo fainali katika mchezo dhidi ya Mamelod Sundowns imeandika barua ya malalamiko kwa CAF kufuatia kukataliwa kwa goli la Azizi Ki dakika ya 58 pasipo Refa wa mchezo huo Raia wa Mauritania, Dehane Beida kwenda kujiridhisha katika VAR.

Kwenye barua hiyo ambayo Yanga imeiandika kupitia kwa Mkurugenzi wake wa sheria Simon Patrick, imewalalamikia Marefa kwa kushindwa kutumia teknolojia ya VAR kupata ufumbuzi, hivyo wanaamini na kulalamika kupitia sheria namba XVI kwamba kuna viashiria vya upangaji wa matokeo ikiwemo pia kitendo cha Refa wa kati kushindwa kwenda kwenye VAR kuangalia utata wa goli hilo licha ya kwamba aliweza kwenda kwenye VAR kuhakiki faulu ya Mchezaji wa Yanga.

banner

Kwenye barua hiyo pamoja na mambo mengine Yanga wameiomba CAF ichunguze tukio hilo kwa undani kwa kutumia ushahidi wa rekodi za VAR na footage za mechi ili kubaini endapo kuna viashiria vya upendeleo kwa Mamelodi vimefanyika na ikijiridhisha kuna upendeleo ichukue hatua kwa kila aliyehusika, iweke hatua madhubuti za kudhibiti tukio kama hilolisijirudie kwenye mechi zijazo na pia ichukue maamuzi mengine ambayo CAF itaona yanafaa chini sheria za mpira za CAF namba XVI kifungu namba 3.

Credit:sportarena_live

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited