Klabu za Yanga sc na Azam Fc zitakutana na klabu za Tabora United na Namungo katika hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Crdb baada ya droo iliyofanyika leo katika makao makuu ya Azamtv Tabata jijini Dar es salaam.
Azam Fc na Yanga sc hazitakutana mpaka fainali endapo zitafuzu hatua za robo na nusu kutokana na droo hiyo ambapo endapo Yanga sc ataifunga Tabora United basi atakutana na mshindi kati ya Ihefu Fc dhidi ya Mashujaa huku Azam Fc akimfunga Namungo sc basi atakutana na mshindi baina ya Coastal union dhidi ya Geita Gold Sc.
Mechi hizo zinatarajiwa kuchezwa kati ya Mei 2-4 mwaka huu ambapo Yanga sc na Azam Fc zote zitaanzia nyumbani na endapo zitapata sare basi zitarudiana ugenenini ili kupata mshindi wa jumla huku pia akikosekana mshindi katika michezo yote miwili basi hatua ya matuta itaamua mshindi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Yanga sc ni mshindi wa taji la ngao ya jamii mara mbili mfululizo ambapo akishinda na msimu huu basi atakua amechukua taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo.