Home Soka Yanga sc,Stars Zatajwa Ubora Afrika

Yanga sc,Stars Zatajwa Ubora Afrika

by Sports Leo
0 comments

Timu ya Yanga sc na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) zimechaguliwa kuwania tuzo ya klabu bora barani Afrika na Timu bora ya Taifa barani Afrika na shirikisho la soka barani Afrika (Caf).

Yanga sc imechaguliwa kuingia kuwania tuzo hiyo kutokana na kufanya vizuri barani Afrika kwa msimu uliopita ambapo ilifanikiwa kutwaa mataji yote ya ndani kisha ikafika hatua ya fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo ilipoteza kwa hesabu ya bao la ugenini dhidi ya Usm Algers.

Katika tuzo hizo Yanga sc itashindana na Mamelod Sundowns,Marumo Gallants(Afrika kusini),Al Ahly Fc (Misri),Wydad Ac na Raja CA (Morroco),Usm Algers na Cr Belouzdad (Algeria) na Asec Mimosas (Ivory Coast) na Us Tunis (Tunisia).

banner

Kwa upande wa Timu ya Taifa ya Tanzania yenyewe imeingia katika tuzo hizo hasa baada ya kufanikiwa kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika (Afcon) yatakayofanyika mwezi januari mwakani ambapo katika tuzo hizo itawania na nchi za Cape Verde, Gambia,Guinnea Bissau,Equatoria,  Guinnea, Morroco, Senegal, Namibia Mozambique  na Mauritania.

Tuzo hizo  zinatarajiwa kutolewa Disemba 11 katika hafla itakayofanyika jijini Marakech nchini Morroco.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited