Home Soka Yanga Wajiamini-Chama

Yanga Wajiamini-Chama

by Sports Leo
0 comments

Kiungo wa Simba sc Cletous Chama amewaasa timu ya Yanga kuelekea mchezo wa marudiano wa kufuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Zesco United ya Zambia mchezo utakaochezwa siku ya jumamosi katika uwanja wa Levy mwanawasa mjini Ndola.

Chama mwenye uraia wa Zambia ambaye alisajiliwa na Simba akitokea Power Dynamos ya nchini humo amewaasa wachezaji wa timu hiyo kujiamini ili waweze kupata matokeo.

“Kitu kikubwa kwanza wanatakiwa kujiamini,lakini wacheze kwa kutulia na kutofanya makosa kwani kama ikitokea wamefanya makosa wanaweza kujikuta wanawapa faida Zesco ya kushinda kwenye mechi hiyo pia wanatakiwa kupunguza presha kwa kua wenzao wapo kwao”.Alisema chama

banner

Yanga inatakiwa kushinda au kutoa sare ya kuanzia mabao 2-2 ili kuweza kufuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika na endapo itapoteza basi itacheza mechi ya mtoani ili kuweza kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited