Yanga sc imeibuka na ushindi wa magoli mawili dhidi ya Friends Rangers katika mechi ya kirafiki iliyopigwa asubuhi ya leo mjini Morogoro katika kambi ya timu hiyo iliyopo chuo cha biblia kilichopo Bigwa mjini humo.
Mabao ya Yanga yalifungwa na Sidney Urikhob dakika ya 38 bao lililodumu hadi mapumziko na kipindi cha pili iliwachukua yanga dakika 23 kupata bao la pili mfungaji akiwa ni nahodha mpya wa klabu hiyo Papy Kabamba Tshitshimbi mabao yaliyodumu mpaka mwisho wa mchezo.
Yanga imekua inaibuka na ushindi katika mchezo yote ya kirafiki ambao imecheza mpaka sasa huku ikifunga magoli zaidi ya 20 na kufungwa magoli chini ya matatu hali inayoonyesha uimara wa safu za ulinzi na ushambuliaji.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.