Home Soka Yanga Yaimaliza Coastal Jioni

Yanga Yaimaliza Coastal Jioni

by Sports Leo
0 comments

Timu ya Yanga sc jana ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Coastal union katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na ligi kuu Tanzania bara iliyosimama kwa ajili ya michuano ya kimataifa ya timu za taifa kuwania kufuzu Afcon mwaka 2021 nchini Cameroon.

Yanga ilian za kujifunga baada ya beki Ally Mtoni kutumbukiza nyavuni mpira wa krosi ambao ulimgonga baada ya kumshinda kipa Farouk Shikalo.

Mabingwa hao wa kihistoria walikosa penati baada ya kiki ya David Molinga kupanguliwa na kipa wa Coastal lakini juhudi za Juma Balinya kumpasia Mrisho Ngasa zilizaa matunda baada ya shuti la Ngasa kujaa nyavuni dakika ya 68 ya mchezo.

banner

Dakika za nyongeza Mapinduzi Balama aliyekua kinara wa mchezo huo alimpasia Papy Tshitshimbi aliyetegua mtego wa kuotea na kujaza mpira wavuni huku pia Balinya akifunga bao la tatu dakika ya mwisho ya mchezo kwa Penati baada ya beki wa Coastal kuunawa mpira.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited