Sasa ni rasmi klabu ya Yanga imemkosa kiungo mkabaji raia wa Rwanda Ally Niyonzima baada ya kiungo huyo kuamua kusaini mkataba wa miaka miwili katika klabu ya Kiyovu Stars inayoshiriki ligi kuu nchini humo.
Kiungo huyo alikua akiwania na klabu ya Yanga ikiwa ni mapendekezo ya benchi la ufundi chini ya mkufunzi Luc Eymael aliyetaka awepo mbadala ya nahodha Papy Tshitshimbi kikosini humo.
Ally Niyonzima mwenye uwezo mzuri wa kucheza nafasi ya kiungo mkabajiamefikia muafaka huo baada ya kutopata muafaka wake mapema wa kujiunga na Yanga ambapo aliambiwa asubiri mpaka finali ya kombe la shirikisho FA ndiyo atalipwa malipo yake ya awali ( advance).
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.