Klabu ya soka ya Yanga imeshindwa kuondoka na alama zote tatu katika mchezo wa mzunguko wa sita wa ligi kuu soka Tanzania Bara mara baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Namungo FC.
Mchezo huo ulifanyika katika dimba la Ilulu huko Lindi ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu hizo kukutana katika uwanja huo wenye historia kubwa nchini katika michezo ya ligi kuu miaka ya nyuma.
Namungo ndio walikokuwa wa kwanza kuwasalimia Yanga kupitia bao la Obrey Chirwa dakika52 ya ,Wanachi walirejea na kusawazisha kunako dakika ya 80 kwa mkwaju wa penati ulipigwa na Mrundi Saido Ntibanzonkiza.
Hata hivyo penati hiyo imelalamikiwa sana na wadau wa soka nchini wakidai haikua halali kwani Feisal Salum hakuguswa na beki wa Namungo,hali inayodhihirisha juendelea kwa makosa ya waamuzi katika michezo ya ligi.
Yanga bado wameendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa na alama 16 alama mbili nyuma ya watani wao Simba SC.