Home Soka Yanga Yatikisa Mji Zambia

Yanga Yatikisa Mji Zambia

by Sports Leo
0 comments

Unaweza kusema mji wa Ndola uliopo nchini Zambia umetikisika baada ya Yanga kutua kibabe mjini humo baada ya kubadili ratiba ghafra baada ya kufika mji wa lusaka nchini humo.

Awali Yanga ilikua ifikie Lusaka na ingeaingia ndola leo ijumaa lakini kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ambapo mji wa ndola na Lusaka imetofautiana baridi hivyo kuwalazimu Yanga kufanya mabadiliko ya ratiba na kuamua kwenda moja kwa moja Ndola.

Kuwasili huko kwa Yanga kuliwatetemesha wakazi wa mji huo ambao wengi ni mashabiki wa Zesco united baada ya awali kutokua na taarifa ya timu hiyo kuwasili mapema zaidi.

banner

Fitna za awali walizokutana nazo wanajangwani hao ni kukatika kwa umeme mara kwa mara katika hoteli ambazo wamefikia hali inayowafanya kuamini kuwa wapinzani wao wanahusika kwa kuwa wanamilikiwa na shirika la umeme la nchi hiyo.

Yanga wanatakiwa kupindua matokea baada ya awali kuruhusu sare ya bao 1-1 jijini Dar es salaam hivyo wanahitaji ushindi wa aina yeyote ama sare ya kuanzia mabao 2-2 katika mchezo huo utakaochezwa katika uwanja wa Levy Mwanawasa jijini humo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited