Home Soka Yanga,Simba Mikoani kipute NPL

Yanga,Simba Mikoani kipute NPL

by Sports Leo
0 comments

Timu za Simba na Yanga zinatarajia kutupa karata zao ugenini katika mzunguko wa sita wa NBC premier league wikiendi hii katika harakati za kusaka pointi tatu muhimu baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa.

Simba imesafiri hadi Mwanza kukutana na Rubu Shooting (Barcelona ya Bongo) siku ya Ijumaa katika dimba la CCM Kirumba majira ya saa kumi jioni,mechi hiyo itakuwa ni ya kwanza kwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo Pablo Franco ambaye ana kazi ya kurejesha furaha Msimbazi.

Katika mchezo huo mratibu wa timu hiyo Abasi ali amethibitisha kuwa watawakosa wachezaji wao Peter Banda na Lary Bwalya huku beki Mkongomani Henock Baka akitumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopata katika mchezo dhidi ya Coastal Union.

banner

Kwa upande wa Yanga wao watakuwepo Mkoani Lindi katika dimba la Ilulu kucheza na wenyeji wao Namungo FC siku ya Jumamosi saa 10 jioni,Wananchi watakuwa wanataka kuendeleza ushindi baada ya kupata alama zote 15 katika mechi za awali.

Mabingwaw hao wa kihistoria itamkosa mshambuaji wake Yacouba Songne ambaye amefanyiwa upasuaji,huku Balama Mapinduzi na Dick Ambundo wakiendelea na programu maalumu baada ya kurejea kutoka kwenye majeruhi.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited