Home Soka Yondani Amtibua Mbeligiji

Yondani Amtibua Mbeligiji

by Sports Leo
0 comments

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema timu hiyo haiwezi kubembeleza mchezaji kwa kuwa anaamini hakuna mchezaji mkubwa kuliko timu

Eymael ametoa kauli hiyo kufuatia mkasa unaomkabili beki kisiki Kelvin Yondani ambaye amekosekana kwenye timu kwa takribani wiki mbili

Mbelgiji huyo amesema Yondani alikosa mazoezi kwa takribani siku sita akitoa sababu kuwa anaumwa huku pia akishindwa kucheza mechi dhidi ya Azam Fc akitoa sababu ya kuumwa tumbo

“Kelvin hakufanya mazoezi kwa siku sita, hata mchezo dhidi ya Azam alidai anaumwa tumbo na hakupatikana hata tulipokuwa tunaenda Singida hatukuweza kumpata hewani simu yake ilikuwa haipatikani”

“Tuliporudi naye akarejea na kusema amepona. Wachezaji wanapaswa kujua kuwa ni lazima twende katika uelekeo mmoja kama timu sichezeshi majina bali nachezesha timu, na hakuna mchezaji mkubwa zaidi ya timu, yeyote ataondoka lakini Yanga itakuwepo,” amesema Eymael

Yondani tayari amerejea kikosini akiendelea na mazoezi na wachezaji wengine hata hivyo jana Eymael alimuweka nje nafasi yake akimtumia Said Juma Makapu

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited