Kuna taarifa za chinichini zinadai klabu ya Yanga sc imempa mechi tatu kocha Mwinyi Zahera ili kuamua hatima yake endapo atashindwa kuipatia ushindi timu hiyo katika mechi hizo.
Taarifa hizo zinadai uongozi wa Yanga umeamua kumpa mechi hizo kocha huyo baada ya kutofurahishwa na matokeo ya mechi ya kwanza ya ligi dhidi ya Ruvu shooting ambapo timu hiyo ilipoteza kwa bao moja licha ya kupata nafasi kadhaa za kufunga.
“Sisi kama viongozi hatuna hizo taarifa kwamba tumempa mechi 3 kocha wetu Zahera Mwinyi asiposhinda mechi tatu tunamtimua”-Rodgers Gumbo, Mwenyekiti Kamati ya Mashindano
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Licha ya uongozi wa klabu hiyo kukana suala hilo lakini taarifa za ndani zinadai mpango huo upo japo hauna nguvu sana lakini mashabiki wa timu hiyo hawaoneshi kufurahishwa na matokeo ya timu hiyo licha ya kufanya usajili wa nguvu.